- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHERIA YA BODI YA KITAALUMA YA WALIMU TANZANIA YATINGA BUNGENI LEO.
BUNGENI DOM: Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaaluma ya Walimu Tanzania wa mwaka 2018 wenye lengo la kuweka muundo wa kisheria wa usimamizi na uendeshaji wa bodi ya kitaaluma ya walimu nchini.
Aidha unalengo la kuweka adhabu ambayo si chini ya shilingi milioni tatu, kifungo cha miaka mitano gerezani au vyote
kwa pamoja endapo mwalimu atakiuka masharti yatakayowekwa kwa mujibu wa sheria hiyo.
Akiwasilisha muswada huo leo waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia profesa Joyce Ndalichako amesema muswada huo una lengo la kuinua hadhi ya taaluma ya ualimu na walimu kwa kuwasajili kulingana na viwango, ueledi na kupewa leseni ya kufundisha katika ngazi stahiki.
Profesa Ndalichako amesema muswada huo umeweka masharti ya uanzishwaji wa bodi, muundo wa bodi, majukumu na mamlaka ya ya bodi.
Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii, Mwenyekiti wa kamati hiyo peter serukamba amesema madhumuni ya sheria yatasaidia taaluma ya ualimu kwa weledi na kuimarisha taaluma ya ualimu kwa kuipa heshima yake.
Wakichangia muswada huo mbunge wa Mwanga profesa Jumanne Maghembe na mbunge wa Nzega Hussein Bashe wameipongeza serikali kwa kuleta muswada huo na kuwaomba wabunge waunge mkono ili kulinda hadhi ya kada ya ualimu.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, zinaeleza kuwa idadi ya walimu wanaofundisha ngazi ya awali, msingi,sekondari na vyuo vya ualimu katika sekta ya umma na binafsi iliongezeka kutoka 257,469 kwa mwaka 2012 hadi kufikia walimu 332,740mwaka 2016.