- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHERIA MPYA YA UZAZALISHAJI WANAWAKE KINGONO KUANZA KUTEKELEZWA
MOROCCO: Sheria mpya ambayo inafanya unyanyasaji wa kingono na Udhalilishaji kuwa ni Uhalifu itaanza kutekelezwa nchini Morocco hivi karibuni.
Sheria hiyo ambayo inajumuisha upigaji marufuku wa ndoa za kulazimishwa, inafuatia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni juu ya kiwango cha udhalilishaji wanawake.
Utafiti mmoja uliofanywa nchini humo, umeonesha kuwa wanawake sita kati ya 10 nchini Moroccan wamepitia manyanyaso hayo.
Matukio ya ubakaji ya hivi karibuni yametangazwa sana katika mitandao ya kijamiii.
Mwandishi wav BBC mjini Rabat amesema sheria hiyo mpya imepokelewa vizuri lakini pia imekosolewa kwa sababu haitoi maana kamili ya unyanyasaji majumbani au marufuku katika vitendo vya ubakaji ndani ya ndoa.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, wale wote watakaotiwa hatiani kwa makosa ya kudhalilisha kingono hadharani iwe kwa kutumia maneno, ama ishara yoyote ya kudhalilisha kijinsia atakabiliwa na hukumu ya kifungo kuanzia mwezi mmoja mpaka sita gerezani na pia faini ya fedha taslimu
Mashirika ya haki za binadamu yanasema kuwa wanawake wengi nchini Morocco wamekuwa ni wahanga wa matukio ya unyanyasaji kingono.
Katika ripoti yake ya mwaka 2015, Shirika la Haki za Binadamu nchini humo limearifu kuwa zaidi ya asilimia 20 ya wanawake nchini Morocco wamekumbwa na matukio ya unyanyasaji wa kingono japo mara moja katika maisha yao
Katika siku za hivi karibuni polisi nchini humo iliwakamata vijana 12 kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 17 na kumtesa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.