- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SETHI ASEMA HAJAONANA NA MKE WAKE KWA ZAIDI YA MIEZI 6
Dar es Salaam: Mshtakiwa anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi Harbinder Sethi leo Agosti 30 ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa ana miezi sita mpaka sasa hajawahi kuonana na mke wake.
Wakili wa Sethi, Dorah Mallaba aliieleza mahakama kuwa bado hawajapata kibali kwa ajili ya mshtakiwa Sethi kuonana na mkewe.
Wakili Mallaba aliiomba mahakama iruhusu hata kwa dakika tano Sethi aonane na mkewe. "Naomba mahakama itumie busara kwa kuwa wake wake yupo hapa mahakamani,β amesema Mallaba Wakili Kombakono baada ya kusikiliza hoja ya wakili Mallaba, aliieleza mahakama kuwa taratibu za kumuona mahabusu zifuatwe.
Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono aliieleza mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi ya Sethi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa. Baada ya Wakili Kombakono kueleza hayo,
Hakimu Shahidi amesema taratibu za kuwatunza mahabusu zipo chini ya Magareza na kama kuna jambo lolote mahususi basi linatakiwa kuletwa mahakamani. Hakimu Shahidi ameiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 13, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia upelelezi utakuwa umekamilika au la. Katika kesi hiyo Sethi na James Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi ikiwamo kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu , kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kutakatisha fedha.