Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:39 am

NEWS: SERIKALI YAZITAKA HALMASHAURI KUKAMILISHA KWA HARAKA UJENZI WA MAABARA.

DODOMA: Serikali imesema ujenzi wa maabara unaendekea katika halmashauri zote ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia masomo ya sayansi.

Akijibu swali la mbunge wa vitu maalum Yosepher Komba aliyetaka kujua (b)’Je, nini , mkakati wa serikali katika kuhakikisha ujenzi wa maabara uanakamilika kwa wakati ili kuimarisha ubora wa elimu’.

Naibu Waziri wa Tamisemi Joseph Kakunda kwa niaba ya waziri wa Tamisemi Selemani Jafo amesema kati ya maabara 10,387 zianahitajika nchini, ujenzi wa maabara 6,287 sawa na asilimia 60.5 ya mahitaji umekamilika.

Mbali na hayo Jafo amezitika halmashauri zote kukamilisha mapema ujenzi uanaondelea kwa kushirikiana , wadau na nguvu za wananchi.