Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 6:54 am

NEWS: SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUPIMA AFYA ZAO MAPEMA.

DODOMA BUNGENI: Serikali imewataka wananchi kufika katika vituo vya afya vya kutolea huduma ili kupima afya zao na kupata ushauri na matibabu mapema.

Akiuliza swali mbunge wa Iramba Mashariki Allan Kiula amesema je, Serikali ina mpangowa kutoa ruzuku ya tiba kwa watanzania wasio na uwezo na wanaougua magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanatumia gharama kubwa ya matibabu’.

Akijibu swali hilo naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watotoDkt. Khamis Kigwangala Amesema sera ya serikali kwa magonjwa sugu yakiwemo yasiyo ya kuambukiza ni kwamba matibabu yanatolewa bila malipo kama vile kisukari, kansa na shinikizo la moyo.

Aidha amesema serikali haitoi ruzuku kwa wasio na uwezo , bali inagharamia matibabu kwa wananchi wanaogundulika kuwa na magonjwa yasio ya kuambukiza bila malipo.