- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAWATAKA WALIVAMIA MISITU YA HIFADHI WAONDOKE MARA MOJA.
DODOMA: Serikali imewataka wananchi waliovamia misitu ya hifadhi ya chenene na chinyami kuondoka katika maeneo hayo mara moja nawatakao kaidi agizo hilo la serikali kwakuendelea kukaa kwenye hifadhi hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mhe, Christina mndeme wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema wapo baadhi ya wananchi amabo wameshaonesha nia juu ya kauli ya serikali yakuwataka waondoke hivyo amewakata ambao bado wapo kuondoka mara moja na serikali haitaongeza muda kwani muda waliopewa tayari umekwisha
Aidha amesema misitu hiyo ndio misitu mikuu wa hifadhi ya maji ya bonde la mzakwe hivyo kuwepo kwa wananchi nakuwepo kwa shughuli za binadamu kama vile kilimo, ufugaji na kukata miti kwaajili ya kuni na mkiaa katika hifadhi hiyo kunahatarisha vyanzo vya maji kwa wilaya na mkoa wa dodoma kwaujumla