- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAWASILISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI.
BUNGENI: Serikali imewasilisha bungeni muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2017 ambapo marekebisho hayo yanalenga kuboresha utekelezaji wa sheria hizo kwa kuondoa upungufu uliojitokeza ikiwemo marekebisho katika sheria ya mahakama ya utatuzi wa migogoro ya Ardhi.
Akiwasilisha hoja kuhusu Muswada huo Mwanasheria mkuu wa serikali George Masaju amesema kuwa kupitia muswada huo utawezesha kufanya marekebisho katika sheria ambazo zimekuwa ni kikwazo katika kutatua masuala mbalimbali ya kisheria
Kwa upande wake msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani na waziri kivuli wa wizara ya Sheria na Katiba Abdalah Mtolea amesema kuwa bado kuna mapungufu makubwa ya sheria hasa katika migogoro ya Ardhi
Baadhi ya wabunge Wakitoa maoni juu ya muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2017 huku wakidai kuwa kupitia muswada huo utaweza kutatua mapungufu mbalimbali ya kisheria
Miongoni mwa miswada inayaotaraji kuwasilishwa katika kipindi hiki cha bunge ni pamoja na muswada wa sheria ya wakala wa meli Tanzania wa mwaka 2017,muswada wa marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017