Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:43 am

NEWS: SERIKALI YAWASHUKIA WAKURUNGEZI WA HALMASHAURI KUHUSU WATU WENYE UALBINO.

DODOMA: Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anayeshulika na walemavu stella Ikupa amewaagiza wakurungezi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa wanaweka katika orodha ya mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi wakati wanapoagiza dawa nyingine kutoka MSD.

Akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Mgeni Jadi aliyetaka kujua mafuta ya ngozi kwa watu wenye ualibino huingizwa kama mafuta ya kaiwaida na kutozwa kodi na kufanya watu hao kushindwa kumudu kuyanunua.

Ikupa amesema serikali inatambua changamoto zinazowakabili watu wenye ualbino na imechukua hatua kadhaa ikiwemo kusambaza vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na watu wenye ualbino.

Ameongeza kuwa katika mwaka 2016/2017 serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi Teknolojiana Elimu ya ufundi imesambaza miwani ya jua 50, mafuta kinga box 100na tayari Bohari kuu ya dawa nchini (MSD) imejumuisha katika orodha ya madawa mafuta kinga kwa ajili ya kuzuia miale ya jua kwa watu wenye ualbino na mafuta hayo hutolewa bila malipo katika hospital ya serikali hapa nchini.

Aidha serikali inaandaa mwongozo wa msamaha wa matibabu (national Health exemption) kwa watu wenye ulemavu wakiwemo watu wenye ualbino.

Mbali na hayo amesema serikali imeondoa kodikwa nyezoza kujimudu kwa watu wenye ualbino (Technical Aids/Appliances) yakiwemo mafuta kinga kwa bidhaa zinazozalisha nje na ndani ya nchi.