Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:46 am

NEWS: SERIKALI YATOA MUDA WA MWAKA MOJA KWA WAWINDAJI.

DODOMA: SERIKALI imetoa muda wa mwaka mmoja kwa wawekezaji wa sekta ya utalii kujipanga kabla mfumo mpya wa ugawaji na umiliki wa vitalu vya utalii kuanza.

Akizungumza leo na wawekezaji wa sekta ya uwindaji mjini Dodoma Waziri wa maliasili na utalii Dk.Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Mfumo huo ambao awali ulikuwa kwa njia ya tenda sasa utakuwa kwa njia ya mnada.

Amesema kuwa kupitia mfumo huo serikali imelenga kuongeza mapato katika sekta hiyo pamoja na kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinalindwa, pamoja na kuongeza tija katika sekta ya utalii.

Amesema katika sekta ya uwindaji wanahitaji watu makini kwa ajili ya uwekezaji hivyo serikali haiwezi kubadilisha utaratibu wa uuzaji wa vitalu kwa njia ya mnada badala yake imeamua kutoa muda wa mwaka mmoja kwa wakezaji hao.

Hata hivyo Dr Kigwangala naeleza jinsi uuzwaji wa vitalu kwa njia ya Mnada utakavyokuwa huku akisema zoezi la hilo linatarajiwa kuanza kufanyika mwezi Julai mwakani ambapo jumla ya vitalu 61 vinatarajiwa kuuzwa katika awamu ya kwanza.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabishara na Wawindaji wa Kitalii Tanzania (TAHOA) ambaye ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya safaris lted Michel Mantheakis akizungumza kwa niaba ya wawindaji nchini amesema wanamuomba Waziri Kigwangalla kuangalia upya utaratibu wa kufuta utaratibu wa utoaji wa vibali hivyo kwani makampuni mengi yamewekeza fedha nyingi.


Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja General Gaudence Milanzi,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dk.Aloyce Nzuki na watendaji mbalimbali wa Wizara hiyo.