- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YATENGA ZAIDI YA BILIONI 1 KWA AJILI YA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI.
BUNGENI DOM: Wizara ya Maji na Umwagiliaji Katika mwaka wa fedha 2018-2019 imesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.302 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji vijijini inayohusisha ujenzi,upanuzi na ukarabati.
Akiongea leo bungeni Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso wakatAkijibu swali la Mbunge wa Mpanda Vijijini,Moshi Kakoso (CCM)
Katika swali lake Kakoso alihoji ni lini Serikali itakarabati visima vilivyojengwa na UNHCR ili kutatua tatizo la maji.
Kakoso amesema kwamba tatizo la maji katika vijiji vya Mlibansi,Mazwe,Mgamsamansi,Ilangu na Kapemba.Je ni lini itakarabati visima vilivyochimbwana UNHCR ili viweze kutatua tatizo la maji katika vijiji hivyo.
Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso,amesema Serikali inaendelea kutekeleza awamu ya pili ya Programu ya sekta ya maji nchini.
Amesema katika mwaka wa fedha 2018-2019 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.302 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji vijijini inayohusisha ujenzi,upanuzi na ukarabati.
Amesema kupitia fedha hizo zilizotengwa itakarabati miradi mbalimbali ya maji katika Halmashauri Mpanda.