- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YATENGA BILION 20.8 KULIPA POSHO ZA WALIMU NA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU.
DODOMA: Serikali imetenga Tsh bilion 20.8 kwa ajili ya posho za walimu pamoja na marekebisho ya sekta ya elimu, nchini ya mpango wa elimu bila malipo.
Akizungumza wakati akifungua mkutano Mkuu wa umoja wa wakuu wa shule za sekondari (TAHOSSA)Tanzania uliofanyika jana mjini hapa Naibu Waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege amesema posho kwa walimu kutasaidia kutambua na kuzingatia majukumu walionayo na mazingira katika kufanya kazi kwa bidii.
Aidha amewataka walimu kutambua majukumu yao nakufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha elimu inasanga mbele.
Akifafanua zaidi amesema licha yakuwepo kwa changamoto ya upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati pamoja na ufundi sanifu wa maabara lakini hadi kufikia Juni 2017serikali iliajiri jumla ya walimu 3599 na kupangwa moja kwa moja shuleni kulingana na mahitaji.
Amesema kati ya walimu hao hisabati na sayansi walikuwa walimu 3462 huku walimu wa ufundi sanifu na maabara ni walimu 137.
"Kutokana na hilo tunaendelda kuajiri walimu wa shule ya msingi na sekondari lengo ni kuboresha sekta ya elimu hapa nchini," amesema Kandege.
Ameongeza kuwa katika mwaka fedha 2017/18 serikali itaendelea kuajiri walimu wengine wa shule za msingi na sekondari ili kuimarisha utendaji wa kazi.
"Ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji aa masomo ya sayansi na ufundi serikali wamenunua na kusambaza vifaa vya maabara kwa shule za sekondari 1692 nchini vyenye thamani ya sh bilon 16," ameongeza kwa kusema Kadenge.
"Tutaendelea kuimarisha maabara katika shule zote zilizobakia niwaombe wananchi waendelee kushirikiana na serikali kukamilisha maabara hizo",amesema Kandege.
Mbali na hayo alizishukuru shule saba za ikiwemo Mtwara, Iyunga,Moshi,Tanga, Musoma, Bwiru,na Ifunda kwa sababu zipo kwenye mpango mkubwa wa uboreshwaji kupitia fedha EP4R na miundombinu itakuwa imekamilika ifikapo mwaka 2020