- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA 2160.
DOM: Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Sulemani Jafo ametangaza ajira za watumishi wapya wapatao 2160.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Jafo amesema kuwa hao ni miongoni mwa watumishi 6785 ambao walipata kibaliMei 30, mwaka 2018 .
‘’Kama tunavyo kumbuka kwamba siku chache zilizo pita tulitangaza jumla ya watumishi jumla ya watumi 4840 kwaajili ya walimu wa shule za msingi pamoja na walimu wachache wa mahitaji maalumu tulibakisha eneo la walimu wa masomo ya sayansi pamoja na hisabati halikadhalika na walimu wengine wa literature pamoja na mafundi sanifu wa maabara, leo naomba kuchukua fursa kuwatangazia ajira hizo mpya 2160’’ amesema Jafo
Aidha Waziri Jafo ameongeza kuwa katika ajira hizo mpya kuna walimu wa masomo ya sayansi na Hisabati wapatao 1900 , walimu wengine wa literature in English wapatao 100 na mafundi sanifu wa maabara wapatao 160 , hivyo walimu hao wanatarajiwa kuripotikatika vituo vyao vipya kuanzia tarehe 23/8 /2018 mpaka tarehe 5/9/2018.
Katika hatua nyingineJafo amesema kuwa jumla ya walimuelfu ishirini mia moja na moja waliweza kutuma maombi yao lakini nafasi walizo nazo ni chache , hivyo kwa wale walimu watakao shindwa kuripoti katikasiku hizo, nafasi hizo zitajazwa kwa walimu wengine.
Pia amesema amesema katika wakati huu wa kujiunga kuna mambo ya msingi ambayo walimu hao wanapaswa kuwa nayo.
Hata hivyo, Waziri Jafoamewaagiza wakurugenzi katika mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha wanawapokea walimu hao na lengo kubwa la kuripoti ni kuhakikishawanakwenda kuwahudumia watoto wa kitanzania, hivyo hatarajiikuona waajiriwa wapya waliotangazwamara tu wanapokwenda kuchukua poshokutoripotikatika vituo hivyo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa atakaye kwenda kinyume na utaratibu.