Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:43 pm

NEWS: SERIKALI YASISITIZA HAKUNA ONGEZEKO LA BEI YA SUKARI.

DOM: Serikali imesema kiasi cha sukari kilichopo nchini kinatosheleza mahitaji ya sukari kwa kipindi cha miezi mitatu mbali na uzalishaji unaoendelea.

Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ametoa kauli hiyo leo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya Hali Sukari nchini ambapo amesema hadi kufikia septemba 5 mwaka huu kiasi cha sukari ya matumizi ya kawaida kilichopo katika maghala ya wenye viwanda,wasambazaji na wafanyabiashara wakubwa ni tani 118.

Aidha Mwijage amesisitiza kuwa hakuna ongezeko kubwa la bei ya sukari kati ya mwezi machi na septemba mwaka 2018

Amewaagiza wenye viwanda nchini kuboresha mfumo wa usambazaji Sukari nchini kwa lengo la kupunguza makali ya bei kwenye baadhi ya Mikoa ikilinganishwa na Mikoa mingine.