- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAOMBWA KUTUNGA SHERIA YAKUTHIBITI BIASHARA YA UUZAJI WA VIUNGO VYA BINADAMU.
DODOMA: Serikali imeombwa kuharakisha mchakato wa utungwaji wa sheria itakayodhibiti biashara ya uuzaji viungo vya binadamu hususan figo.
Imeelezwa kuwa uwepo wa sheria hiyo itazuia biashara ya uuzaji viungo vya binadamu, hasa figo ambayo imeshamiri katika nchi za bara la Asia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Egid Mabofu, baada ya Hospitali ya Benjamini Mkapa kufanikisha upandikizaji figo kwa wagonjwa watatu.
"Kuuza kiungo chako ni kosa kama inavyoeleza Azimio la Istanbul la mwaka 2008, ambalo limepiga marufuku uuzwaji viungo vya binaadamu kwani ni kuudharirisha utu na kuondoa dhana ya binaadamu kuwa wote sawa na wanastahili kuishi," amesema Professa Mabofu.
Aidha Profesa Mabofu amesema kuwa kuuziana viungo ni kinyume na haki za binaadamu, hivyo lazima kuwepo kwa sheria itakayodhibiti kutokea uuzaji wa viungo ikiwemo figo.
Akifafanua kuhusu upandikizaji figo kwa wagonjwa, amesema wagonjwa watatu waliopandikizwa figo pamoja na ndugu waliowapatia figo afya zao zimeimarika na wameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.
"Mwanzoni hawakuwa na nguvu pamoja na muda wa kutosha kumudu majukumu yaliyokuwa yakiwakabili kwa sababu ya ugonjwa wa figo ila baada ya upandikizwaji figo afya zao zimeimarika," amebainisha.
Akizungumza awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mpaka, Dk. Alphoce Chandika, amesema huduma ya upandikizaji figo itakuwa endelevu.
"Hatua hiyo imewezesha wananchi kupata huduma bora za afya na hatimae kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa," amesemaDk Chandika,.
Mmoja wa wachangiaji figo, Eunis Kishosha, ametoa wito kwa Watanzania kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji kupandikiziwa figo.
Amesema hali yake ni nzuri na anaweza kuendelea na shughuli zake za kawaida, hivyo amewataka Watanzania kuondokana na kasumba kuwa kujitolea figo kwa mgonjwa kuna madhara.