Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:44 am

NEWS: SERIKALI YAKITAKA CHAMA CHA TLS KUACHANA NA UANAHARAKATI WA KISIASA.

DOM: Naibu katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Amon Mpanju amekitaka chama cha wanasheria Tanganyika TLS kufanya kazi za kuwahudumia wananchi kulingana na taaluma yao kwa mustakabaliwa taifa badala ya kugeuka wanaharakati wa kisiasa.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na katibu huyo wakati akifungua mafunzo ya wakufunzi wa mafunzo ya wasaidizi wa kisheria nchini.

Mpanju amesema serikali ipo tayari kukosolewa na kuelekezwa na mawakili ili kujenga nchi kwa faida ya watanzania wote na vizazi vijavyo lakini kama watazingiata taaluma zao na kuacha uanaharakati.

Akizungumzia kuhusu wasaidizi wa kisheria Mpanju amesema wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuwasaidia wananchi kupata haki yao huku wakiwa katika mazingira magumu.

Mkurugenzi Mtendaji TLS Kaleb Gamaya amesema kuwa wananchi wana matatizo mengi yanayohitaji wasaidizi wa kisheria ili kupata haki yao ambayo wakati mwingine hayana ulazima kwa kupeleka mahakamani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mawakili mkoa wa Dodoma Mery Munisi amesema mwanzoni ilikua vigumu kwa mawakili kuwakubali wasaidizi wa kusheria kwani waluthani wanakuja kuchukua nafasi yao.

Wasaidizi wa kusheria nchini wamekua wakifanya kazi kubwa ya usuluhishi wa migogoro na kuwasaidia wananchi namna ya kudai haki zao hasa katika maeneo ya vijijini.