- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA SHULE KONGWE
Serikali mejipanga kuhakikisha shule zote za umma hususan kongwe zinarudi kwenye ubora wake kama zamani kutokana na hivi karibuni kuonekana hazifanyi vizuri kitaaluma na kukosa mvuto.
Hayo yamesema leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo wakati wa kikao kazi cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Taifa ya kidato cha sita kwa mwaka 2018, jijini hapa.
Aidha Kikao hicho kilichojumuisha wakuu wa shule za sekondari 30 zilizofanya vizuri kwenye mtihani hiyo.
Waziri Jafo amesema mwenendo wa shule hizo sio mzuri kwa kipindi kirefu ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
“Miaka ya nyuma tulishuhudia mtoto asipochaguliwa kwenye shule za umma familia inakuwa na majonzi kwanini mtoto wetu hajachaguliwa shule ya serikali kwa kuwa mwenendo wa shule za umma ulikuwa ndo kioo cha Taifa,”amesema.
Akiendelea kufafanua waziri Jafo amesema kwasasa zimekosa mvuto na kufanya baadhi ya wazazi wenye watoto wenye ufaulu mkubwa kuwapeleka shule za binafsi na wenye ufaulu mdogo kuachwa shule za umma wanazochaguliwa.
“Lengo la serikali kwasasa linafanikiwa na kwa mwaka huu shule tatu za umma zimeingia 10 bora ambapo ni Kisimiri, Mzumbe na Kibaha, hivyo kwa mwaka 2019 tunataka kwenye 10 bora ziwepo shule sita za umma kwenye matokeo ya kidato cha sita,”ameongeza kwa kusema.
Pia Jafo amesema lengo ni kuzifanya zirudi kwenye hali ya zamani, na ifikapo mwaka 2020 shule zisizopungua tano ziingie kumi bora kwenye matokeo ya kidato cha nne.
Mbali na hayo amewataka wakuu wa shule hizo kuhakikisha wanajiandaa kugombea nafasi ya tatu kwenye 10 bora kitaifa na kuwataka kuhakikisha daraja la ufaulu linakuwa la kwanza na kuondoa daraja la pili.
“Kaandaeni timu nzuri ya ushindi ili muweze kufanya vizuri kitaaluma tunataka Rais John Magufuli katika uongozi wake ajivunie shule za umma kurudi kwenye ubora wake,”alisema.
Akizungumza mara baada ya kikao hicho , Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Msalato, Line Chanafi amesema siri ya mafanikio ni juhudi na maarifa ya pamoja kati ya walimu na wanafunzi na wamekuwa wakishauri na kutatua matatizo ya wanafunzi.
Kwa upande wake , Mkuu wa shule ya sekondari Kibaha Chrisdom Ambilikile alisema wamejipanga kuhakikisha kunakuwa na matumizi mazuri ya muda, nidhamu na kusimamia ufundishaji kwa wanafunzi.