Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:50 am

NEWS: SERIKALI YAFUNGUKA KUHUSU UHABA WA DAWA.

DODOMA: Serikali imewatoa haofu wanachikuhusiana na tatizo la upungufu wa dawa kwa kusema kuwa kwa sasanchi haina upungufu mkubwa wa dawa na inafanya kila liwezekanalo kuhakisha kuwa dawa zote muhimu zinapatikina katika kila kituo cha afya.

Aidha imesema hali hiyo imetokana na serikali kutenga fedha nyingi za kununua dawa tofauti na zamani na hivyo wanachi hawapaswi kubaki na mawazo ya awali kuwa kuna uhaba wa dawa

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto UMMY MWALIMU ametoa taarifa hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Siha dk GODWIN MOLEL lilihoji kwanini kunakuwa na dawa zilizoharibika na kuteketezwa wakati nchi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa hasa maeneo ya vijijini.

UMMY akijibu swali hilo amesema takwimu za kuwepo kwa upungufu wa dawa nchini ni za zamani kwani kwa sasa serikali ya awamu ya tano imefanya kazi kumbwa kuhakikisha dawa zinapatikana katika vituo vyote vya afya nchini.