- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAAHIDI KUTOWAVUMILIA WEZI.
DODOMA: Serikali imesema haitawavumilia watendaji wanaochangia kuhujumu vyama vya ushirika kwa kufanya ubadhilifu na vitendo vya wizi wa mali za ushirika.
Hayo yamesemwa na Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Tito Haule wakati wa maadhimisho ya siku ya vyama vya ushirika wa Akiba na mikopo Duniani yaliyofanyika kitaifa jana mjini hapa.
‘’Kwahiyo changueni viongozi watakao weza kuongoza taasisi hizi kwa weledi na kwa uaminifu mkubwa’’, amesema.
Kwa upande wake Katibu mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuviwezesha vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo kufanya kazi zake vizuri kwa ajili ya kutoa huduma zake kwa wanachama na jamii inayozunguka.
‘’Hivyo natoa rai kwenukutumia fursa hii vizuri ili kuhakikisha kwamba vyama hivi vinaendeshwa kwa kuzingatia malengo na madhumuni ya kuazishwa kwake’’, amesema.
Katika hatua nyingine Mathew ameitaka jamii kujiunga na vyama vya ushirika wa akiba na mikopo ili kujipatia maendeleo kiuchumi na kupunguza umasikini nchini.
Baadhi ya wananchi akiwemo Fatuma Shilimo amesema waliojiunga katika vyama vya akiba na mikopo wamesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa jamii kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopa hali itakayosaidia kupunguza umaskini na hatimaye kukuza uchumi wa nchi.
‘’Na vilevile ushirika unasaidi kwa sababu uko tofauti tofauti kuna wengine wanadili na wafanyakazi na kilimo kuna baadhi ya ushirika unadumu na wafanyakazi kwahiyo tunavyokutana hivi tunasaidiana kutatua changamoto’’,amesema.
kilele cha maadhimisho hayo kinataraji kufanyika mapema October 19 mwaka huu ambapo wadau kutoka mikoa mbalimbali wanakutana katika maadhimisho hayo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo kwa mwaka 2017 inasema Jiunge na SACCOS kutimiza ndoto zako