Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 8:43 pm

NEWS: SERIKALI YAAHIDI KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI SOKO LA MWANI.

BUNGENI DOM: Serikali imeahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mpango Madhubuti wa Maendeleo ya Mwani ambao umeainisha mikakati ya kutatua tatizo la soko la mwani ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Zaynabu Vulu aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuboresha zao hilo na inamsaidiaje mkulima wa mwani kupata soko la uhakika hususan nje ya nchi.

Ulega amesema pia itasaidia wananchi kuingia mikataba yenye tija na makampuni ya mwani pamoja na kutafuta masoko mapya nje ya nchi ili kusaidia wakulima kupata bei bora zaidi.

Ulega amesema kilimo cha zao la mwani kinachofanyika katika mwambao wa Bahari ya Hindi ni miongoni mwa shughuli za sekta ndogo ya ukuzaji viumbe maji ambapo jumla ya tani elfu 1,329.5 za zao la Mwani zenye thamani ya shilingi milioni 469.8 zilivunwa mwaka 2017/2018 huku tani elfu 1,197.5 zenye thamani ya shilingi milioni 412 zilivunwa na kusafirishwa nje ya nchi kwa mwaka 2016/2017.