- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : SERIKALI YA UFARANSA YAPIGA MARUFUKU WAISLAMU KUSWALI SALA YA IJUMAA MJI WA PARIS
Serikali ya Ufaransa yawawekea Waislamu vizuizi vipya wasiweze kusali Sala ya Ijumaa katika mji wa Paris
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerard Collomb amesema ni marufuku kusali Sala la Ijumaa katika eneo la Clichy kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Paris.
Kufuatia hatua iliyochukuliwa mwezi Aprili mwaka huu ya kuufunga msikiti maarufu wa Clichy, Waislamu wa eneo hilo wamekuwa wakisali Sala ya Ijumaa barabarani kulalamikia uamuzi huo.
Waislamu nchini Ufaransa wanasema serikali haijawapatia eneo mwafaka la ardhi kwa ajili ya kujenga msikiti mpya na kwamba licha ya kukubaliana na udharura wa suala hilo hadi sasa haijachukua hatua yoyote kuhusiana na jambo hilo.
Jumuiya moja ya Waislamu ya mjini Paris imetangaza kuwa Sala ijayo ya Ijumaa itasaliwa katikakati ya mji mkuu huo wa Ufaransa.
Katika Sala ya Ijumaa iliyosaliwa tarehe 10 ya mwezi huu wa Novemba watu wapatao 100 wakiwemo wanasiasa wa Ufaransa walikusanyika mahala inaposaliwa sala hiyo na kuimba kwa sauti kubwa wimbo wa taifa wa Ufaransa ili kuzuia kutekelezwa ibada hiyo tukufu ya kisiasa na kimaanawi ya Kiislamu.
Kuenezwa hisia za chuki na hofu dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika nchi za Magharibi kumewafanya Waislamu wa nchi hizo wakabiliwe na mbinyo na mashinikizo makubwa katika kutumia haki yao ya uhuru wa kuabudu.../