Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:37 pm

NEWS : SERIKALI YA BURUNDI YAUNGA MKONO MAREKEBISHO YA KATIBA

Serikali ya Burundi yaunga mkono marekebisho ya katiba,ambapo huenda Rais wa hivi sasa,Nkurunzinza akapewa mihula mingi zaidi

Serikali ya Burundi imeidhinisha marekebisho ya katiba ambayo yatatoa fursa ya kurefushwa kwa uongozi wa Rais Pierre Nkurunzinza, kulingana na maelezo ya maafisa waandamizi wa serikali hiyo.

Burundi Pierre Nkurunziza (picture-alliance/dpa/C. Karaba)

Huenda uongozi wa rais Pierre Nkurunzinza ukarefushwa kwa miaka mingine 14. Hii ni baada ya serikali ya Burundi inayokabiliwa na migogoro kuidhinisha marekebisho ya katiba ambayo yatatoa fursa ya kurefushwa kwa uongozi wake, kulingana na maelezo ya viongozi wakuu.

Mawaziri, waliokutana jumanne katika kikao maalumu, waliafiki misingi ya mageuzi yaliopendekezwa.

Katiba ya sasa ya taifa la Burundi inatokana na makubaliano ya amani ya mwaka wa 2000, yaliyosainiwa katika mji wa kaskazini mwa Tanzania wa Arusha ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 12 ambayo ilisababisha vifo zaidi ya 300,000.

Kwa mujibu wa afisa ambaye hakutaka jina lake litajwe, mabadiliko yanayopendekezwa hayatagusa viwango vya mgao wa madaraka kwa misingi ya kabila na jinsia, katika serikali, bunge na polisi, lakini hakuna popote makubaliano ya amani ya Arusha yanakotajwa.

Makubaliano ya Arusha yanasema wazi kwamba hakuna rais anayeweza kutawala nchi kwa zaidi ya miaka 10.

Lakini Burundi inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa, uliochochewa wakati makundi ya upinzani, yalipoamua kutetea yaliokubaiwa kwenye mkataba wa Arusha, kwa kupinga uchaguzi mnamo Aprili 2015 ambayo ulimwezesha Nkurunziza kubakia madarakani kwa kipindi chengine cha miaka mitano.