- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA 289 IFIKAPO 2020.
DOM: Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) imejipanga katika kuhakikisha inajenga vituo vya kutolea huduma hasa vituo vya afya vipatavyo 289 kabla au ifikapo mwaka 2020.
Lengo la dhamira hiyo ni kupunguza vifo vitokanavyo na sababu mbalimbali.
Hayo yameelezwa hivi karibuni jijini Dodoma hapa na Mkurugenzi wa huduma za afya,ustawi wa jamii na lishe kutoka OR- TAMISEMI dokta Ntuli Kapologwe wakati akitoa mada katika kikao kazi cha waganga wakuu wa Mikoa,Wilaya na waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini.
Ametaja mambo ambayo yamefanyika katika kipindi cha mwaka 2017/2018 mbali na ujenzi wa vituo vya afya kuwa ni ujenzi wa nyumba za watumishi zipatazo 390 na majengo takribani 1,500 yamejengwa na serikali nchi nzima na kuanzisha mfumo wa mshitiri mteule ambaye jukumu lake ni kuhakikisha anapeleka dawa,vifaa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya pindi vifaa hivyo vinapokuwa vimekosekana katika Bohari kuu ya dawa (MSD).
Akizungumzia kuhusu idara yake amesema pamoja na mambo mengine ina jukumu lao ni kuhakikisha huduma za Ustawi wa Jamii zinazohusu Wazee, watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na uimarishaji wa huduma za ustawi wa Jamii ngazi ya Jamii zinaimarika.
Utekelezaji wa masuala ya Idara hiyo ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe yameainishwa katika Sera ya Afya ya Mwaka 2007, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa Nne (HSSP IV -2015-2020),Mpango wa Maendeleo endelevu (SDG -2015 -2030) na kwenye Ilani ya CCM ya Mwaka 2015-2020.