- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU DOM.
DODOMA: Serikali imesema itaendelea kuboresha miundombinu iliyopo ya hudumaza kijamii na miundombinu ya barabara , maji, umeme na mawasiliano ili kuwavutia wageni na mataasisi ya kimataifa kuweza kuhamia Mkoani Dodoma .
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa wakati wa haflaya ufunguzi rasmi wa ofisi ya umoja wa mataifa Dodoma.
Majaliwa amesema baadhi ya watendaji wanaogopa kuhamisha watoto wao na wenza wao ili kuanza maisha mapya kutokana nachangamoto zilizopo katika mkoa Ddoma.
‘’Napenda kuwatoa hofu kwamba Dodoma ni mahali pazuri pa kuishi na kuna fursa nyingi,’’amesema Majaliwa.
Aidha ameongeza kuwa serikali imejipanga kujenga mji bora na wa kisasa Dodoma unaoendana na mahitaji na mfumo wa kisasa wa miji bora Duniani.
‘’Serikali imeupatia Umojawa Mataifa eneo kubwa na la kutosha ili muweze kujenga majengo mazuriya kisasa kwa ajili ya Mashirika yote ya Umoja wa Mataifa ikiwemo UNDP,UNFPA,FAO,ILO,WHO,na UN-WOMEN,’’ameongeza kwa kusema Majaliwa.
Hata hivyo amesema hadi sasa watumishi 2,346 wameshahamia Dodoma na mwisho mwa mwezihuu mheshimiwa Makamu wa Rais Samia Suluhu atahamia Dodoma na mwaka kesho 2018 Rais atahamia Dodoma.
Mbali na hayo alisema Umoja wa Mataifa unachangia jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo katika Nchi yetu kupitia mipango mbalimbali miongoni mwa mipango iliyotekelezwa katika miaka ya karibuni ni mpango wa kwanzawa Umoja wa Mataifa wa misaada UN Development Assitance Plan (UNDAP 1) Uliotekelezwa kuanzia mwaka 2011 hadi 2016.
Pia Mpango wa pili wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa unatekelezwa kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 changamoto kubwa ya utekelezaji wa mipango hiyo ni ufinyu wa Bajeti.
‘’Naamini Viongozi wa Umoja wa Mataifa wataipatia ufumbuzi wa changamoto hiyo ili kuiwezesha Tanzania kuendelea kupata misaada,’’amesema Majaliwa .
Awali akizungumza waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Dk Augustine Mahiga amesema Majukumu ya umoja wa mataifa ni kunachangia kwa kiwango kikubwa katika kuleta maendeleo hali ya amani na usalama duniani, Umoja wa Mataifa bi mfano mzuri wa kuigwa barani Afrika katika kudumia amani.