Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 8:32 pm

NEWS: SEREKALI YAWATAKA WAKUU WOTE WAMIKOA KUJENGA VIWANDA 100

Dar es salaam: Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo ameagiza kila Mkuu wa Mkoa katika eneo lake kujenga viwanda vipya 100 ndani ya mwaka mmoja kuanzia Desemba 2017 mpaka Decemba 2018

Waziri Jafo amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo Desemba 2018 kila mkoa uwe umejenga viwanda vidogo vidogo na vya kati visivyopungua 100 katika ngazi ya mkoa.

Jafo amesema kuwa mikoa ya Tanzania Bara pekee inatakiwa kuwa na viwanda vipya vidogo na vya kati visivyopungua 2,600 ifikapo Desemba 2018.

Serikali imekusudia kufikia nchi ya uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda huku akiwataka wakuu hao kuibua viwanda vidogo na vya kati kwa kuhamasisha ushiriki wa viongozi ndani ya mikoa na wananchi katika maeneo yao ya utawala