Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:41 am

NEWS: SEREKALI YATOA TAMKO KUPASUKA KWA BOMBA LA GESI DAR ES SALAAM

Dar es salaam:Jana jioni kulitokea mlipuko mkubwa wa gesi uliolipuka na kuteketeza nyumba na mali kadhaa eneo la Hospitali ya Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam ambapo mlipuko huo umetokana na Bomba la gesi kutoka Songo Songo, Lindi/Mtwara kwenda Ubungo, Dar, kupasuka baada ya mafundi wa Dawasco waliokuwa wakiweka miundombinu ya kupitisha mabomba ya maji, kulitoboa bomba hilo kimakosa.


Akiongea kwa niamba ya Dawasco kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuulizwa swali na mwananchi juu ya tukio hilo Katibu mkuu wa Maji na Umwagiliaji Prof. Kitilia Mkumbo amesema kuwa tukio hilo lilitokea kwa bahati mbaya lakini wanashukuru kwakua hali ilidhibitiwa na hakuna aliyepoteza maisha katika tukio hilo

''Hii ilikuwa bahati mbaya sana. Bomba dogo la TPDC na mafundi wetu wa DAWASCO hawakulitegemea mahala pale. Tunashukuru hali imedhibitiwa na hakuna maisha yaliyopotea. Tutafanya tathmini kuhusu mali zilizoathirika. Pongezi kwa kikosi cha zima moto na wananchi''

Nae kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wakati akiongea na wananchi wa eneo hilo amesema suala hilo limetokea kutokana na uzembe watendaji “Tunajua ni kosa la baadhi ya watendaji kutokuwa na ramani, sababu unapotaka kufanya mradi mwingine lazima uwe na ramani, wenzetu hawakusoma ramani, lazima ujue hapa walipitisha nini.” aliongea Makonda