Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:55 pm

NEWS: SEREKALI YASEMA HAKUNA MGAO WA UMEME

Dar es salaam: Serikali kupitia Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani imesema hakuna mgawo wa umeme nchini na kwamba tatizo la kukatika kwa umeme linalojitokeza hivi sasa katika maeneo mengi litamalizika Desemba 15, mwaka huu.

Dkt. Kalemani ameongeza kwamba tatizo hilo linatokana na kufanyika kwa marekebisho ya mitambo iliyochakaa kwa kudumu kwa takribani miaka 40 sasaAidha, amefafanua kuwa lengo la marekebisho yanayofanywa ni kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na mitambo itakayowezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika wakati wote

Aidha, Waziri ameeleza kuwa Serikali inaendelea na mchakato wa kumpata mkandarasi atakayejenga mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge, uliopo katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji unaotarajiwa kuzalisha megawati 2,100 kwa mkupuo, mradi ambao unatarajiwa kwa kiasi kikubwa kutatua kero ya umeme iliyodumu kwa muda mrefu nchini.