Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:54 am

NEWS: SEREKALI YASEMA HAITAKI KULUMBANA NA MH. LISSU

Dar es salaam: Jana baada ya mbunge wa Singida mashariki na Rais wa chama cha mawakili Tanganyika TLS Tundu lissu kutoa tuhuma na mapendekezo yake juu ya serekali ya Tanzania inavyoshughulikia tukio la kushambuliwa kwa risasi mnamo september 7 mwaka jana Nyumbani kwake Area D mjini Dodoma, Serikali ya Tanzania kupitia Msemaji wake Dokta Hassan Abbasi, amesema serikali haiwezi kumjibu Lissu kwa sasa

"Mhe Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni busara kulumbana naye kwa sasa. Tunaendelea kumuombea apone haraka."

serekali imekuwa ikisema kuwa, inaendelea na uchunguzi kubaini waliomshambulia mwanasiasa huyo wa upinzani.

Jana kwenye mahojiano maalum na vyombo vya Habari Tundu Lissu amesema shambulio dhidi yake lililotokea Septemba saba mwaka 2017 lilikuwa sawa na mauaji ya kisiasa.

Lissu ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa upinzani alishambuliwa na watu wasiojulikana akiwa nje ya makazi yake Mkoani Dodoma, nchini Tanzania baada ya kuhudhuria kikao cha bunge.

“Mimi sio mfanyabiashara na nimeshambuliwa katika eneo wanaloishi viongozi wa bunge na ambalo lina ulinzi, kwa maoni yangu shambulio hilo ni sawa na mauaji ya kisiasa,”amesema mbunge huyo na kueleza kuwa alimiminiwa risasi 16 kwenye mwili wake.

Baada ya kukamilisha hatua ya kwanza ya matibabu, Mbunge huyo ambaye pia ni rais wa Mawakili wa Tanganyika, anatarajiwa kwenda Ulaya kwa matibabu zaidi.