- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAKAMATA TANI 20 ZA KOROSHO
Waziri wa Kilimo na chakula, Japhet Hasunga,ametangaza kuzikamata Tani 20 za korosho kutoka ghala la mtu binafsi la Olam lililoko mkoani Mtwara.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, Waziri Hasunga, amesema korosho hizo zilikabidhiwa katika Chama cha Msingi cha Mnyawi kwa lengo la kuchanganywa kinyemela na zile zinazopelekwa kwenye maghala makuu.
“Jana tulikamata tani 20 zilizokuwa zimepenyezwa katika vyama vya msingi, tusingependa lijirudie hivyo, wananchi wawe makini kuhakikisha korosho zinazoletwa katika vyama vya msingi ni zile za Watanzania ili korosho yetu peke yake iendelee kununuliwa na Serikali,” amesema Hasunga.
Amesema korosho zitakazokamatwa kutoka nje au kuingizwa kinyemela kwenye vyama vya msingi zitataifishwa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Jumanne wiki hii tani nyingine tisa zilikamatwa katika eneo la Newala baada ya kuingizwa kinyemela toka nchini Msumbiji.
Aidha juzi pia yalikamatwa magunia 152 ya korosho katika Wilaya ya Nanyumbu yaliyoingizwa nchini kutoka Msumbiji.