- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAKAMATA TANI 1.2 ZA SAMAKI NA KUZIGAWA BURE
Bukoba: Serekali Mkuani kagera kupitia Idara ya uvuvi mkoani humo imekamata samaki aina ya sangara kiasi cha tani 1.2 wenye thamani ya Sh10.3 milioni ambao walipatikana kwa njia za uvuvi haramu na walikuwa wakitoroshwa kutoka nchini kwenda nchini Uganda kwa ajili kuuzwa.
Kwamujibu wa Ofisa mwandamizi wa ulinzi wa rasilimali za uvuvi Kanda ya Ziwa, Didasi Magembe ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa Novemba 9,2018 kwa waandishi wa habari katika viwanja vya ofisi za idara hiyo katika manispaa ya Bukoba mkoani humo.
Magembe amesema kati ya samaki hao wapo wanapaswa kutumiwa na wapo ambao wako chini ya sentimita 50 na wengine zaidi ya sentimita 85 wanaoruhusiwa kwa mujibu wa sheria na kwamba kiwango hicho kimegawiwa kwa taasisi mbalimbali zikiwemo baadhi ya shule za sekondari.
Amesema samaki hao wanavuliwa kwa kutumia zana za uvuvi haramu kama makokoro, timba, ndoano na mitumbwi au boti huku wanaohusika wakitumika usiku kuingia ndani ya Ziwa Victoria
"Tumejipanga kuhakikisha tunalinda rasilimali ndani ya ziwa kwa kufanya doria za mara kwa mara huku wanaotuhumiwa wakifikishwa mahakamani au kutozwa faini kwa mujibu wa sheria," amesema Magembe.
Aidha ofisa mwandamizi wa uvuvi mkoani Kagera, West Mbembati amesema katika kipindi cha kuanzia Oktoba 20 hadi jana Novemba 8, 2018 wamekamatwa wavuvi haramu 41 kati yao wanne wamefikishwa mahakamani na 37 wametozwa faini na kunyang’anywa zana zao.