Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:45 pm

NEWS: SEREKALI YAANZA KUGAWA BILIONI 2 KWA WAKULIMA WA KOROSHO

Serekali ya Tanzania kupitia Benki ya kilimo Tanzania(TADB) imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 2 kwa wakulima wa korosho wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma katika malipo ya kundi la kwanza la watu ambao tayari wamehakikiwa kupitia vyama vya msingi na vyama vya ushirika.Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema TADB imeanza kulipa wakulima wote walioakikiwa katika mikoa tajwa kupitia vyama vyao vya Msingi na ushirika kwa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wakulima moja kwa moja kupitia akaunti zao.


"zoezi la ulipaji limeanza jana na kwasasa tumewafikia wakulima zaidi ya 2168 kutoka mikoa mitatu tulionza nayo hivyo tunategemea kuendelea kulipa mpaka kufikia jumatatu tutakuwa tushalipwa wakulima wengi sana kama ilivyoagizwa na Rais Dk . John Pombe Magufuli kutaka fedha hizo ziende kwa wakulima moja kwa moja bila ya makato"amesema Waziri Hasunga.