- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YA KENYA YAPINGA MAANDAMANO YA WAPINZANI (NASA)
Nairobi: Serikali ya Kenya imetangaza kupiga marufuku maandamano ya wafuasi wa upinzani NASA katikati ya miji nchini humo.
Waziri wa Usalama na Mambo ya ndani Fred Matiang'i, amesema maandamano hayo hayataruhusiwa katikati ya jiji la Nairobi, Mombasa na Kisumu.
Matiang'i ameongeza kuwa hatua hii imechukuliwa baada ya baadhi ya waandamanaji wa upinzani kupora mali ya watu katika miji hiyo siku ya Jumatano.
Aidha, Waziri huyo amefafanua kuwa serikali haiwezi kuzuia maandamano kwa sababu ni haki ya wakenya kama ilivyoanishwa kikatiba, kuandamana ila inachofanya, ni kuepusha mali ya watu kuporwa na kuharibiwa.
“Tunafanya hivi ili kuzuia uharibifu wa mali ya watu na kuwalinda Wakenya wengine wasiotaka kuandamana,” alisema.
“Maandamano ni haki ya kila mtu kwa sababu hilo lipo kwenye Katiba ya nchi,” aliongeza Matiang'i.
Hata hivyo, waandalizi wa maandamano ya upinzani wakiongozwa na kiongozi wa vijana katika muungano huo Benson Musungu, wamepuuzilia mbali marufuku hayo na kusisitiza kuwa yataendelea kama ilivyopangwa siku ya Ijumaa.
Musungu amesema maandamano ya Ijumaa yataendelea kama ilivyopangwa na kila siku kuanzia Jumatatu ijayo.
Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga ambaye ametangaza kujiondoa kwenye Uchaguzi huo kwa kile alichosema kuwa, hajaridhishwa na maandalizi ya Tume ya Uchaguzi, yupo ziarani nchini Uingereza.
Tume ya Uchaguzi inasema, uchaguzi wa tarehe 26 utaendelea kama kawaida lakini wanasheria na wachambuzi wa siasa wanaotofautiana kuhusu uhalali wa Uchaguzi huo.