Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:56 pm

NEWS: SEREKALI KUTUMIA WATAALUMU WA NDANI KUPANGA MIJI

Dar es salaam: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali haitajihusisha na kampuni za wataalamu wa mipango miji kutoka nje ya nchi (Tanzania), badala yake itaendelea kuwatumia wa ndani kutokana na uwezo wao kwa sasa.

"Tumeona kazi nyingi zimefanywa na wataalamu wetu wa ndani, takriban asilimia 90 ya kazi zote za uandaaji wa mipango kamambe imeandaliwa na wataalamu hawa, kwa hiyo hakuna haja ya kutumia wengine kutoka nje," amesema Lukuvi.

Lukuvi amesema hayo leo Alhamisi Oktoba 26,2017 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa Bodi ya Usajili ya Wataalamu wa Mipango Miji jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo umeshirikisha wajumbe wa bodi 150 kutoka kampuni za wataalamu wa mipango miji Tanzania.

Nayo Bodi ya Mipango miji, imesajili wataalamu 306 kati yao wataalam 16 wamefutiwa vyeti vya usajili kutokana na makosa mbalimbali.
Katika hatua nyingine, amesema urasimu unaotokana na sheria za nchi umekuwa kikwazo katika miradi inayotekelezwa na halmashauri.