- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI KUFUNGA RADA MPYA VIWANJA VYA NDEGE
Dar es Salaam: Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema imeanza utaratibu wa kufunga rada mpya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana baada ya kuwasili kwa mitambo ya rada hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari alisema mradi wa ujenzi wa rada mpya nne utagharimu Sh67.3 bilioni na utachukua miezi 18 11kukamilika.
Tanzania ina rada moja zamani ya kuongozea ndege iliyonunuliwa kwa Gharama ya Tsh 40 Bilioni mwaka 2002 ambayo uwezo wake wa kufanya kazi umepungua kutokana na kasi ya mabadiliko katika sekta ya usafiri wa anga Duniani.
Rada ya zamani ilinunuliwa kupitia kampuni ya BAE System ya Uingereza lakini iliibua utata mkubwa baada ya kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo, Andrew Chenge baada ya kubainika bei hiyo ilikuwa kubwa kinyume na bei halisi.
Kwasasa Kampuni ya Thades ya Ufaransa ndiyo iliyoshinda tenda ya ufungaji wa rada nne mpya zitakazoiangaza Tanzania ambazo zitafungwa kwenye JNIA, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Mbeya (Sia) na Uwanja wa Ndege Mwanza.
“Hizi rada zitafungwa kila moja kwa wakati wake. Hii ya Dar es Salaam inaanza kufungwa leo (jana) na itakamilika baada ya miezi mitano kuanzia sasa na ikikamilika inawashwa na itakayofuatia itakuwa vivyo hivyo hadi ikamilike yote minne,” alisema Johari.
Alitaja faida zitakazopatikana kutokana na mradi huo kuwa ni pamoja na kuiwezesha Tanzania kuboresha utoaji wa huduma za kuongoza ndege, kukuza sekta ya usafiri wa anga katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuwa zitawezesha pia ndege nyingi kupita katika anga la Tanzania kwa kuwa litakuwa salama zaidi.
Waziri wa zamani wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba wa mradi huo alisema, “Hivi sasa ndege zinazoruka urefu wa futi 24,500 anga la Tanzania hawazioni, rada za Kenya ndizo zinaziongoza, lakini hizi zikishafungwa hali hiyo itatengemaa.”