Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:49 am

NEWS: SEREKALI IMEZUIA SHIRIKA LA HAKI ZA BINAADAM KUTOA RIPOTI YA UNYANYASAJI

Dar es salaam: Serekali imelizuia shirika la haki za Binaadam la Human Right watch kuzindua Ripoti inayoonesha unyanyasaji wa watumishi wa ndani wa kitanzania wanofanyakazi za ndani nchi za njee katika nchi za falme za kiarabu. Ripoti hiyo itaangaza namna ya wanawake wengi wa kitanzaninia wanvyonyanyaswa na waajiri wao katika nchi hizo.

Upande wa serekaili umegoma kutolewa kwa ripoti hiyo kwa sababu ya shirika hilo kutofuata utaratibu wakati wa kufanya utafiti huo. kwahiyo serekali inaona kuwa huenda kunavitu vingi vitaripotiwa ambavyo havina usahihi.

Siku za hivi karibuni wanawake wengi kutoka nchi za Afrika mashariki wamewahi kuripoti kuwa wanafanyiwa matendo ya kinyama Kama kulazimishwa kufanya matendo ya ngono, kupigwa, kubakwa, kunyimwa ujira wao, kunyang'anywa hati za kusafiria pindi wanapokwenda kuajiriwa kwenye nchi hizo.