Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:25 am

NEWS: SEREKALI IMEPANGA KUTUNIA BIL 1.2 KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI NCHINI

Ruvuma: WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa serekali imepanga kutumia Shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa miji 25 Tanzania Bara na Visiwani.

Kauli hiyo ameitoa leo Octoba 24 wakati akizindua mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga akiwa katika ziara yake kikazi mkoani Ruvuma.

Profesa Mbarawa amesema mradi huo ni hatua ya Serikali kufikia lengo la kufikia asilimia 90 kwa miji mikuu ya wilaya itakapofika mwaka 2020.

Amesema mradi huo utabadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi wa Mbinga sio tu kwa kutoa huduma ya majisafi na majitaka kwa wananchi. Pia, ni muhimu kwa shughuli za kila siku za kiuchumi zinazofanyika katika mji huo.

Vilevile, Profesa Mbarawa ameipongeza Mamlaka ya Maji ya Songea Mjini (SOUWASA) kwa kazi nzuri ya kusimamia mradi huo mpaka umekamilika.

Mradi huu upo chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya mji wa Mbinga (MBIUWASA) ulianza kujengwa Mei, 2017 chini ya mkandarasi Almasi General Supplies Ltd ya Songea na kuanza kutoa huduma ya maji kwa mji wa Mbinga Februari, 2018 umegharimu Shilingi Bilioni 1.029.