Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:52 am

NEWS: SEDIT WATUA DODOMA.

DODOMA: Imeelezwa kuwa kwa miaka 13 Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kuhamasisha wananchi wa kipato cha chini kujiunga katika Vikundi kupitia mfumo wa Ushirika wa akiba na Mikopo (VICOBA) (Social and Economic Develoment Intiatives of Tanzania ( SEDIT) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanikiwa kuwa na Vicoba zaidi ya 4000 katika halmashauri zaidi ya 40.

Pia Vikundi hivyo vinawanachama zaidi ya 80000 wakiwa na wamejijengea mitaji yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 30.0.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi Mtendaji wa SEDIT Filbert Sambagi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya juma la Vicoba na maonyesho ya biashara za wanavicoba.

Amesema mafanikio hayo yameleta changamoto zaidi katika uhitaji wa mitaji zaidi ya biashara, teklonojia na rasilimali bora za uzalishaji masoko na elimu zaidi ya usimaminzi wa biashara.

Naye Meneja wa Bank ya NMB tawi la Dodoma Harold Lambileki Ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuwatumia na kuwaamini mawakala wa benk wa Mitaani kwakuwa wamesajiliwa na serikali na wanafanyakazi kihalali.

Kwa upande wake Afisa mwandamizi huduma na Elimu mlipakodi Mkoa Dodoma Barnabas John Masika amesema mwaka 2016 serikali ilipitisha kuanza kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara wadogowadogo [wamachinga] waliweka utaratibu kuwa wafanyabiashara hao watambulike na wasajiliwe lengo ni kutoa elimu kwa wadau hao.

Maadhimisho ya Juma la Vicoba na maonyesho ya biashara za wanavikoba yataanza tarehe 5/11 hadi tarehe 10 Novemba mwaka huu katika viwanja vya Nyerere Square kauli mbiu ya maonyesho hayo ni ‘’Vicoba Kwa Mapinduzi Ya Kilimo , Viwanda Na Uchumi Wa Tanzania’’.