- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SAUD ARABIA YAMTIMUA BALOZI WA CANADA NA KUSITISHA KUFANYA BIASHARA NA NCHI HIYO
Nchi ya Saudi Arabia imesitisha kufanya biashara na uwekezaji wowote mpya na nchi ya Canada na Kumtimua Balozi wa nchi hiyo nchini Saudia kwa kile inachodai kuwa inaingiliwa na nchi hiyo masuala ya ndani ya taifa hilo la Ghuba.
Kwenye ujumbe kadhaa kupitia mtandao wa twitter wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Saudi Arabia, ilisema itamfukuza balozi wa Canada na kumuita balozi wake aliye Canada.
Hatua hii inakuja baada ya Canada kusema kuwa ina wasi wasi kutokana na kukamatwa kwa wapiganiaji kadhaa wa haki za binadamu.
Kati ya wale waliokamatwa ni mpiganiaji wa haki za wanawake nchini Saudi Arabia Samar Badawi.
Bi Badawi amekuwa akitoa wito wa kumalizika mfumo wa wanaume kuwasindikiza wanawake kila wanapokwenda.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema haiwezi kamwe kukubali kuingiliwa kwa masuala ya ndani ya nchi yao.
Ilizungumzia taarifa ya wiki iliyopita ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Canada iliyoitaka Saudi Arabia kuwaachilia mara moja wanaharakati wa kupigania haki za wanawake.
wanaharakati wa saudia
Wizara nchini Saudi Arabia ilitaja hatua hiyo ya Canada kama shambulizi dhidi ya nchi yake ikisema kuwa sasa:
- Itasitisha biashara mpya na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.
- Itamuamrisha balozi wa Canada kuondoka nchini humo ndani ya saa 24.
- Itamuita balozi wake kutoka Canada.
- Itakuwa na haki ya kuchukua hatua zaid.
Serikali ya Canada hadi sasa haijatoa taarifa yoyote kufuatia hatua hizo za kidiplomazia za Saudi Arabia.
Kukamatwa huko ni kinyume na hatua zikizopigwa na serikali mwaka huu chini ya uongozi wake mrithi wa ufalme Mohammed bin Salman.
Alilijozolea sifa mwaka uliopita wakati alitangaza kuondolewa marufuku ya miongo kadhaa ya kuwazuia wanawake kuendesha magari.
Wanaharaki wa kutetea haki za wanawre wakiweo wale waliokuwa wamefungwa kwa kukiuka marufuku hiyo walisherehekea uamuzi huo.
Lakini pia waliapa kuendelea kupigania sheria ambazo walizataja kuwa za kibaguzi.
Wanawake ni lazima wafuate sheria kali za mavazi, wasijihusishe na wanaueme wasio na mahusiano nao na wasindikizwe au wawe na ruhusa iliyoandikwa kutoka kwa mwanamume ambaye ni lazima awe ni baba, mume au ndugu ikiwa wanataka kusafiri ng'ambo, kufanya kazi na kupata huduma ya afya