- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SAMIA AZITAKA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUTENGA MAENEO KWA AJILI YA WAJASIRIAMALI.
DODOMA: Makamu Wa rais Samia Suluhu ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo na kuweka mifumo lasimi itakayowawezesha wajasiriamali wadogo waweze kujiajiri.
Suluhu ametoa kauli hiyo leo wakati Wa uzinduzi Wa Sera ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2017 na mkakati Wa utekelezaji wake uliofanyika mjini hapa.
‘’Wawe na maeneo ambayo hawata kwenda kusumbuliwa na mgambo, wala mapolisi wa jiji wawe na maeneo yanayotambulika haya ni maeneo ya wajasiriamali ,’’amesema.
Suluhu ameongeza kuwa miongoni mwa maagizo mengine ni pamoja na halmashauri zote kuhakikisha zinaunda vikundi vya mikopo, kuongeza ubunifu ili kupunguza athari wanazozipata wananchi nchini.
‘’Kuhakikisha halmashauri zote kutenga fedha asilimia 10, tano kwa wanawake na tano kwa wanaume,’’amesema.
Mbali na hayo amebanisha changamoto katika sera hiyo ni ongezeko la idadi kubwa ya watu ,ongezeko la riba kwenye taasisi zinazohusika na mikopo, ukosefu wa mfumo wa sheria.
‘’Jambo kubwa linaloturudisha nyuma ni ukubwa wa riba kwenye mikopo kiasi kwamba wajasiriamali wadogo kushindwa kukopa,’’amesema.
Aidha aliwataka wadau kuwa na ushirikino na wananchi katika kutoa elimu juu ya suala la mkopo ili kuweza kupunguza umasikini nchi.
‘’ Mafanikio tuliyoyapata ni kutengeza ‘socialnetwork’ mtandao wa kijamii ambayo itaingizwa kwenye bima ya afya,’’alisema.
Amesema Ili kukuza sekta ya fedha nchi wadau na taasisi mbalimbali nchi lazima kuwepo na ushirikiano baina yao.
Awali akizungumza waziri wa fedha na mipango Dk Philipo Mpango alisema changamoto zingine ni kutokuwepo kwa mfumo wa kusimamia watoa huduma na hakuna vigenzo au riba za utoaji wa mikopo.
Hata hivyo amesema lengo la sera hiyo ni kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini na luwafikia watu masikini (fukala) ili kujikwamuwa na kukuza uchumi wa Taifa..
Mchakato wa sera ya huduma ndogo za fedha kwa mwaka 2017 na mkakati wa utekelezaji wake ulianza mnamo mwaka 2000.