- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SABABU ZA KUJITOA WAKILI WA KESI YA VIONGOZI WA CHADEMA
Dar es salaam: wakili Jeremiah Mtobesya, aliyekuwa anatetea viongozi waandamizi wa Chadema wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 112, kujitoa katika kesi hiyo. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ameendelea kuonyesha kutoridhishwa kwake na uendeshaji wa Hakimu Wilbard Mashauri
"CHADEMA tunaheshimu Mahakama zetu, hatujawahi na hatutadharau mahakama zetu, lakini kuna baadhi hawafuati sheria inaonekana wazi wanatekeleza maagizo badala ya kufuata sheria" alisema Mbowe
Wakati akizungumza na wanahabari Jana tarehe 23 Agosti, 2018, Mbowe alisema kitendo cha wakili huyo kujitoa katika kuwatetea kinadhihirisha kile alichokiita kuwa, Hakimu Mashauri anaendesha kesi yao kwa kufuata maagizo yaliyotoka juu badala ya kufuata sheria.
Mbowe ameeleza kuwa, malalamiko yao kuhusu kutokuwa na imani na Hakimu Mashauri hayamaanishi kama wanaogopa kufungwa, bali hawataki kufungwa kwa makosa wasiyokuwa na hatia nayo.
Mbowe amedai kuwa, Hakimu Mashauri anaiendesha kesi hiyo haraka haraka kana kwamba anapokea mashinikizo kutoka juu.
“Tuliwahi kufikia hatua ya kumkataa hakimu kutokana na mwenendo wake unaonyesha kama anaendesha kesi kwa mashinikizo. Hatua hii imechosha mawakili wetu. Wakili amejitoa bado hakimu akataka kesi kesho iendelee,” amesema.
Wakili Mtobesya alijitoa katika kesi hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuyatupilia mbali maombi ya washtakiwa ya kutaka kesi hiyo iahirishwe. Ili kusubiri maombi yao ya rufaa yaliyopo katika mahakama ya rufani.
Viongozi hao wa Chadema wapatao tisa wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo ya kufanya mkusanyiko kinyume na sheria.