Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:38 pm

NEWS: RUSHWA BADO GUMZO CHINI

DODOMA: Imeelezwa kuwa rushwa ni moja kati ya changamoto inayokabili mabadiliko ya kiuchumi nchini ili kukomesha hali hii mapambano makubwa yanahitajika.

Akiongea na wanahabari mjini Dodoma ,Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)mkoa wa Kagera Yahaya Mateme amesema kuwa rushwa bado ni tishio kwa mabadiliko ya uchumi na hivyo jitihada za kuikomesha zinahitajika.

Amesema,vijana kama nguzo ya taifa wanapaswa kusimama kidete kuhakikisha suala la rushwa na na vichocheo vyake linakomeshwa kwa maendeleo ya Taifa.

Mbali na hayo amesema kuwa ili kuikomesha rushwa inayotokana na umaskini pamoja na tamaa kwa baadhi ya viongozi ,Serikali inapaswa kuelekeza jicho zaidi kwenye sekta ya kilimo ili kuwakwamua vijana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya Amani Kajuna amesema kuwa vijana wanapaswa kujitambua na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.

Naye mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Sylivesta Yared amesema kuwa Serikali inapaswa kutengeneza nafasi nyingi kwa vijana zaidi ili kuweza kuwakwamua na umasikini uliokithiri kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kujiajiri na kutosubiri kuajiriwa na kwamba Serikali ya chama cha Mapinduzi inaamini mabadiliko ya hali ya juu ikiwa kila mtu atashiriki kikamilifu katika kujituma.