Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:40 am

NEWS: RUGE ALIA NA UWONGOZI WA DAR ES SALAAM KUIBANIA FIESTA

Dar es salaam: Mkurugezi wa Vipindi na uzalishaji wa kituo cha habari cha Clouds Media Group Ruge Mutahaba ameonesha masikitiko yake juu ya uwongozi wa mkoa wa Dar es salaam kuliwekea ufinyu wa muda Tukio kubwa la burudani la Fiesta 2017, Akihojiwa kwenye kipindi ya Clouds 360 kinachorushwa majira ya asubuhi Ruge amesema kuwa anashangaa kwamba tukio la fiesta linazaidi ya miaka 15 likifanyika katika mikoa tofauti toufaiti ndani ya Tanzania kwa muda wa saa za usiku na kunabaadhi ya mamlaka ya mikoa inaongeza mpaka asubuhi.

''Ikiwa ni mwaka wake wa 16 sasa, Fiesta hufanyika hadi saa za usiku na wakati mwingine huenda zaidi ya hapo. Kinachotofanyika huwa ni Wakuu wa Mikoa viongozi pamoja na mamlka zote, kwa kuzingatia uhitaji wa Wananchi wengi, ukubwa na tija ya Fiesta kwa nchi, wanaamua kuongeza muda. Hilo lipo katika mamlaka yao, limefanyika miaka yote na limefanyika mwaka huu katika mikoa 16 tuliyopita. " Katika Mikoa mingine Makamanda wa Polisi wa mikoa hiyo, Wakuu wa mikoa na mamlaka zote huwa wanatushauri kupeleka TigoFiesta2017 hadi asubuhi. Wanatuambia inasaidia sana kiusalama. Hapa Dar imekuwa tofauti, tunaamini Mamlaka zinaona huo ndio muda sahihi na tunashukuru sana kwa namna walivyojipanga" - alisema Ruge

Kauli hiyo ya Ruge imekuja mara baada ya Taarifa ya awali kutoka kwenye mamlaka ya mkoa Dar es salaam iliyowataka waandaaji wa Fiesta 2017 kuishia saa 6 usiku badala ya saa 9 au mpaka asubuhi kama ilivyo pangwa, ambapo baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alipowatembelea kuwapa pole uwongozi wa Clouds Media alisema amewaongezea muda wa saa 1 kuisha kwa tukio hilo mpaka saa 7 usiku kauli ambayo Ruge ameipinga nakusema kuwa hakuna muda wowote waliongezwa kwa sababu sheria ya baraza la sanaa Basata inawataka waishie saa 7 usiku

"Sheria tunayoifahamu (Kanuni za Baraza la Sanaa, kifungu namba 27 kifungu kidogo cha 2 B) inaruhusu kwenda hadi saa 7:00. Inaa maana tukiambiwa tuishie saa 7 hakuna muda tulioongezewa. Sasa tumeomba kuongezewa muda lakini iikishindikana, TUTAFANYA HIVYO HIVYO. Tuko vizuri sana, hatutakwama mahali, tutapewa nguvu na Watanzania. Kinatakachokosekana ni wale wasanii 20 ambao itabidi tuwapunguze alisema Ruge.

Ruge amesema kuwa swala hilo ameliachia kwenye mamlaka ya wananchi wapenda burudani kwamba wao wataamua kuwapa sapoti vijana wenzao "Uzuri katika hili hakuna siasa hata kidogo, hapa ni vijana wataamua kuwapa nguvu vijana wenzao (wasanii wanaowapenda). Tutapewa nguvu na vijana wanaojua kwamba hii movement ya muziki ilianza siku nyingi, na haiwezi kukwama sasa hivi" Ruge