- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RPC DOM AWASHUKIA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA.
DODOMA: Wenyeviti wa serikali za mitaa mkoani Dodoma wametakiwa kudhibiti uhalifu katika maeneo yao kwa kuwachukulia hatua Kali watu watakajihusisha katika uvunjifu wa amani wakati wakushusheherekea sikukuu ya mwaka mpya.
Rai hiyo imetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto wakati akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa kuhusu kuunda vikundi vyakuzuia vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha hakuna mtu anaechoma matairi, kuvunja chupa barabarani ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kumbi za starehe zinafungwa kwa muda muafaka pamoja na kuzuia disko toto kwani ni kinyume cha sheria na zinaharibu watoto.
Aidha amewataka wazazi kuhakikisha wanazuia uhalifu kwakuwakanya vijana wao kujihusisha na uhalifu na kijana atakaekamatwa na mzazi wake atakamatwa kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 na hapa anaeleza zaidi
Akizungumza kwenye mkutano huo mwenyekiti wa wenyeviti mkoa wa Dodoma Matwiga Matwiga amesema wataendelea kushirikiana na jeshi la polisi na itakua si uungwana endapo uhalifu utaendelea kutokea kwenye mitaa hasa kwakipindi ambacho serikali iko mkoani hapa hivyo amewaada wananchi kutoa taarifa pale watakapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani
Sanjari na hayo afm imezungumza na baadhi ya wenyeviti waliohudhuria mkutano huo na kusema kuwa wameyapokea maagizo yote waliyopewa nakuongeza kuwa wataendelea kuboresha ulinzi katika maeneo yao kwakutumia polisi jamii ili wananchi waweze kusherekia mwaka mpya kwa amani kama ilivyokuwa wakati wa skukuu ya Noel.