- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC DOM AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUSIMAMIA KWA WELEDI ZOEZI LA UKUSANYAJI WA MAPATO.
DOM: Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge ameziagiza hamashauri zote Mkoani hapa pamoja na wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ili kuhakikisha mkoa huo unaingiza mapato kwa kiwango kikubwa ikiwa ni kigezo cha kupima uwezo wa utendaji kazi wao.
Dk Mahenge ametoa agizo hilo wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya ya Dodoma na Bahi walioapishwa mkoani humo.
Katika hatua nyingine Dk Mahenge amewataka wakuu wa wilaya za mkoa huo kuhakikisha wanasimamia maendeleo katika maeneo yao ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi pamoja na kuinua kiwango cha elimu katika mkoa huo huku akibainisha kuwa kitaaluma maendeleo ya mkoa huo hayaridhishi.
Kwa upande wake Erick Simon ambaye ni mkuu wa nyanda za juu kusini ofisi ya maadili amewataka viongozi waliopishwa kuzingatia maadili na miiko ya viongozi kaatika utekelezaji wa majukumu yao.
Nao wakuu wa wilaya walioapishwa kutumikia Wilaya ya Dodoma na Bahi ambao ni Patrobas Katambi sambamba na Mwanahamisi Mkunda wameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea maendeleo wananchi