Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:50 pm

NEWS: RC DODOMA AZITAKA TAASISI ZA DOM KUWAWEZESHA VIJANA KIMAARIFA.

DODOMA: Taasisi zilizopo mkoani Dodoma,zimetakiwa kuwawezesha vijana katika vitu vinavyotumia maarifa ili kuweza kutatua changamoto zilizopo mkoani hapa ikiwa ni pamoja na kilimo cha maarifa.

Hatua hii imekuja mara baada ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge alipofanya ziara kwa mara ya kwanza katika chuo cha ufundi VETA ikiwa ni hatua ya kukagua shughuli za maendeleo zinazofanywa na chuo hicho.

Akiongea mara baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo ya chuo hicho,Dk Mahenge amesema taasisi zilizopo mkoani hapa zinapaswa kushirikiana kutatua changamoto zilizopo ili kuifikia azma ya serikali ya awamu ya tano ya viwanda.

Aidha,mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa vijana wengi mkoani hapa hawana ujuzi wa elimu ya viwanda na hivyo kumtaka mkuu wa chuo hicho kujipanga kuandaa mafunzo ya ujuzi kwa manufaa ya viwanda vinavyotarajiwa kuanzishwa.

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Ramadhan Mataka amesema kuwa kwa nafasi yake atahakikishaanatekeleza ushauri uliotolewa na mkuu wa wa mkoa na kwamba taasisi yake imejipanga kuongeza uzalishaji kwa kupitia kozi za muda mfupi ili kuwafikia walengwa wengi zaidi.

Mbali na hayo amesema,katika kuendana na sayansi na tekinolojia chuo hicho kinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia ambapo vilivyopo ni vile ambavyo havijaboreshwa.

Hata hivyo Mataka ametumia nafasi hii kuwataka mafundi wote wenye ujuzi mbalimbali kujikita zaidi katika kuboresha kazi zao na kutokubali kuchukulia kila kitu kuwa ni kawaida.

Naye karani kazi wa chuo hicho Benard Mkenda amesema chuo cha VETA kipo kwa ajili ya maendeleo ya jamii na katika kudhibitisha hilo wameanzisha jengo la karakana kwa ajili ya mafunzo ya hatua ya pili ya ubobezi wa samani bora.