- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC DODOMA ALAANI KITENDO CHA WAZEE KUKATWA FEDHA ZA TASAF
DODOMA: Kufuatia siku chache mtandao wa muakilishi kuripoti juu ya malalamiko ya wazee wa kata ya Hombolo Manispaa ya Dodoma kukatwa fedha zao za TASAF na kuingizwa katika mfuko wa Bima ya afya ya CHF Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana amekemea vikali suala hilo na kuiagiza halmashauri husika kuhakikisha wazee hao wanarudishiwa fedha zao haraka iwezekanavyo.
Mh Rugimbana ameyasema hayo wakati akizungumza na muakilishi leo ofisini kwake na kuongeza kuwa TASAF ni mfumo uliowekwa na Serikali kwa ajili ya kuwasaidia wazee masikini hivyo kuwakata fedha hizo kwa kisingizio cha kuwapatia kadi za Bima za CHF haikubaliki kwani wazee hao pia wanastahili kupatiwa matibabu bure.
Aidha kufuatia kitendo hicho Rugimbana ametoa siku saba kwa halmashauri ya manispaa ya Dodoma kuhakikisha inalifuatilia suala hilo na wazee wote wakiokatwa fedha zao ili hali wana sifa ya kupata matibabu bila malipo warudishiwe fedha zao.
Kwa upande wake mratibu wa TASAF Mkoa wa Dodoma Bogit Samhenda amesema si haki kwa wazee hao kukatwa fedha wanazopewa na TASAF kwa nguvu hivyo wananchi wanatakiwa kutoa taarifa za kiongozi atakayefanya kitendo hicho ili aweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Wazee hao walitoa malalamiko yao wiki moja iliyopita pindi mtandao wa muakilishi ulipowafikia ambapo walizielekeza lawama zao kwa Mwenyekiti wa mtaa wa Hombolo Bwawani A Livingstone Yona Mlugu kwa kudai kuwa huwakata fedha wanazopewa na TASAF kwa nguvu na kuwaeleza kuwa wanapaswa kuchangia katika mfuko wa Bima ya afya ya CHF