“Mkuu wa Mkoa hakupaswa kumuweka ndani diwani, kwa sababu alitekeleza maagizo ya kikao cha halmashauri na agizo hilo liltolewa mwaka jana na Waziri wa Maliasili na Utalii na tukaamua kumpa kibali kingine cha ujenzi mtu huyo aliyebomoloewa.” amesema Meya wa Iringa mjini.
Aidha Meya huyo alidai Mkuu wa Mkoa wa Hapi kutumia baadhi ya fedha ambazo zilikuwa zimelekezwa kwenye miradi mingine kutumika kwenye ziara yake aliyoipa jina la Iringa mpya iliyodumu kwa siku 20 madai ambayo Mkuu wa mkoa Hapi alitaka aulizwe Mkurugenzi wa Manispaa.
Hapi aliagizwa kukamatwa kwa diwani wa viti maalum Selestin Kokumbya siku ya ijumaa ya wiki iliyopita.