- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA YEMEN AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI
Rais wa zamani wa nchini Yemen Ali Abdullah Saleh ameuawa katika mapigano na washirika wake wa zamani,
Mashirika ya habari yanayodhibitiwa na waasi wa Houthi yameripoti taarifa kutoka kwa maafisa hao wakitangaza "mwisho wa mzozo wa wanamgambo wahaini na kiongozi wao".
Taarifa pia kutoka kwenye chama chake Bw Saleh cha General People's Congress pia wamethibitisha kwamba amefariki, kwa mujibu wa Al Arabiya TV.
Picha na video zilizosambazwa mtandaoni zimeuonesha mwili wa mwanamume anayefanana na Bw Saleh ukiwa na kidonda kichwani.
picha ya Rais wa zamani wa nchini Yemen Ali Abdullah Saleh baada ya kupigwa risasi
Hadi kufikia wiki iliyopita, wafuasi wa Bw Saleh walikuwa wanapigana pamoja na wapiganaji wa jamii ya Houthi dhidi ya rais wa sasa wa Yemen Abdrabbuh Mansour Hadi.
Lakini uhasama wa muda mrefu wa kisiasa pamoja na mzozo kuhusu udhibiti wa msikiti mkuu katika mji mkuu wa Sanaa unaodhibitiwa na waasi vilichangia mapigano makali ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 125 na wengine 238 kujeruhiwa tangu Jumatano usiku.
Jumamosi, Bw Saleh aliahidi "kufungua ukurasa mpya" na Bw Hadi anayesaidiwa na muungano wa mataifa yanayoongozwa na Saudi Arabia iwapo majeshi hayo yangeacha kuishambulia Yemen na kuondoa marufuku ya kutoingiza chakula na bidhaa Yemen.Pande hizo mbili zilipokea kwa furaha tamko la Bw Saleh.
Lakini waasi wa Houthi walitazama hilo kama "mapinduzi" dhidi ya "ushirika ambao hakuwahi kuwa na imani nao."
Watu zaidi ya 8,670 wameuawa na wengine 49,960 kujeruhiwa tangu majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yalipoingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe Machi 2015, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Mzozo huo pamoja na marufuku ya kutoingiza chakula na bidhaa Yemen ambayo imekuwa ikitekelezwa na Saudi Arabia pia umewaacha watu 20.7 milioni wakihitaji kwa dharura msaada wa kibinadamu, na pia kusababisha hitaji kubwa zaidi ya chakula cha dharura duniani.
Aidha, kulitokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao unaaminika kusababisha vifo vya watu 2,211 tangu Aprili.