Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:43 pm

NEWS : RAIS WA URUSI,VLADIMIR PUTIN ATAKA SILAHA ZA KEMIKALI KUANGAMIZWA

Rais Putin ataka kuangamizwa kikamilifu silaha za kemikali dunianiRais Putin ataka kuangamizwa kikamilifu silaha za kemikali duniani

Rais wa Russia ameitaka jamii ya kimataifa ifanye juhudi za kuangamiza kikamilifu silaha za kemikali duniani.

Rais Vladimir Putin ametuma barua kwa mnasaba wa kufunguliwa kikao cha 22 cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya Inayopinga Matumizi ya Silaha za Kemikali (OPCW) katika mji wa The Hague Uholanzi akitaka kuangamizwa kikamilifu silaha hizo.

Katika barua yake hiyo Rais wa Russia amezitaka nchi zote zinazomiliki silaha za kemikali zifanye jitihada za kuangamiza haraka silaha zao na kuzitolea pia wito nchi ambazo hazijajiunga na azimio linalopiga marufuku silaha za kemikali zijiunge mara moja.

Silaha za kemikali za Marekani

Tarehe 27 mwezi Septemba mwaka huu Russia iliangamiza mabaki ya silaha zake za kemikali; kitendo ambacho kilitajwa na Rais Putin wa nchi hiyo kuwa ni hatua kubwa katika juhudi za kuwa na dunia inayoheshimu utekelezaji kamili wa majukumu na yenye utulivu zaidi. Kikao cha 22 cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya Inayopinga Matumizi ya Silaha za Kemikali (OPCW) kilianza shughuli zake mjini the Hague Uholanzi jana Jumatatu tarehe 27 Novemba na kitaendelea hadi Disemba Mosi