- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA URUSI AGUSWA NA AJALI YA MV NYERERE ATOA RAMBIRAMBI
Moscow: Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa salaam za Rambirambi na pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Kufuatia Ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyouwa zaidi ya watu mia mbili ishirini na nne (224) katika kijiji cha Ukara wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza mnamo septemba 20 mwaka huu.
Salaam hiyo ni Kupitia taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Moscow Sept. 21, 2018 siku moja baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Putin ameungana na viongozi wengine wakubwa Duniani kutoa salaam zao za pole kwa nchi ya Tanzania wengine ni Papa Francies, Rais Kagame wa Rwanda, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Musseven wa Uganda, Rais wa China Xi jinping na wengine.
Jana kumefanyika Maziko ya miili 9 ya watu waliopoteza roho zao katika ajali hiyo, maziko ambayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
Aidha tukio hilo lilihudhuriwa na baadhi ya wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya, maofisa wa serikali, vyama vya siasa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Miili hiyo tisa imezikwa kwa makubaliano baina ya serikali na familia za wahanga waliopoteza maisha huku serikali ikiahidi kujenga mnara wa kumbukumbu ya ajali hiyo mbaya kuikumba Tanzania katika miaka ya karibuni.
Miili mingine 172 ilitambuliwa na jamaa wa wahanga na kuchukuliwa kwa ajili ya maziko katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Katika hatua nyingine serikali ya Tanzania imeahidi kuunda tume ya uchunguzi kuhusu mkasa huo na kwamba wale wote watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema serikali ina mpango wa kuimarisha huduma ya usafiri katika visiwa mbalimbali vilivyomo katika wilaya ya Ukerewe.
Kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake kutoka Bugorola kwenda Ukara kilizama Septemba 20 kikiwa na zaidi ya watu 250 na kufikia leo juhudi za uokozi zimefanikiwa kuokoa watu 41 na kuopoa miili 224.
Imeandikwa na Deyssa h. Issa
Imehaririwa na Merry Mgawe
Muakilishi publisher