Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:34 am

NEWS : RAIS WA UFARANSA ALIA NA BIASHARA ZA UTUMWA ZILIZOPO NCHINI LIBYA

Rais wa Ufaransa alalamikia utumwa nchini Libya

Rais wa Ufaransa alalamikia utumwa nchini Libya

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesisitizia udharura wa kung'olewa kikamilifu magenge ya magendo ya binadamu nchini Libya.

Macron amesema hayo baada ya kuonana na Rais Alpha Condé wa Guinea Conakry ambaye ndiye mwenyekiti wa hivi sasa wa Umoja wa Afrika na kuwaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na Alpha Condé kwamba, biashara ya binadamu nchini Libya ni jinai dhidi ya ubinadamu ambayo imeongezeka katika orodha ya jinai nyinginezo zinazotendeka nchini humo kama vile ugaidi.

Magendo ya binadamu janga jingine kubwa nchini Libya

Amesema, maafa hayo ya kibinadamu nchini Libya yanayaingizia magenge ya magendo ya binadamu faida ya Euro bilioni 30 kila mwaka.

Kwa upande wake, Jean-Yves Le Drian, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa ametishia kuwa, iwapo Libya haitachukua hatua za kukabiliana na kukomesha uhalifu huo mkubwa wa magendo ya binadamu, basi itawekewa vikwazo Siku chache zilizopita vyombo vya habari viliripoti kuwa wahajiri wanapigwa mnada na kuuzwa hadharani kama bidhaa nchini Libya huku kukiwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa za kuzuia jinai hiyo.